WISE ONE ATOA SIRI YA KUSHINDWA KUIMBA ZAIDI KWENYE WIMBO WA BEN POL(BADO KIDOGO) - NGELANGELA NEWS

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday, January 4, 2018

WISE ONE ATOA SIRI YA KUSHINDWA KUIMBA ZAIDI KWENYE WIMBO WA BEN POL(BADO KIDOGO)

Msanii wa muziki kutoka Dodoma Wise one ambaye ameshirikishwa kwenye wimbo wa msanii wa rnb Ben Pol uliopewa jina kidogo ameelezea sababu yakushindwa kuimba zaidi kwenye wimbo huo aliopewa nafasi.
Image may contain: 1 person, sunglasses and text
Akizungumza nakipindi cha Micharazo time msanii huyo ambaye amesikika akiimba mistari miwili kwenye wimbo huo amesema watu wengi wanadhani kuwa Ben Pol ndiye ambaye alimwambie aimbe mistari miwili kwa lengo lakuogopa kufunikwa au kubana lakini si kweli kwani aliukuta wimbo huo ukiwa umeshamaliziki tyari na Ben Pol hakuhitaji kuotoa huo wimbo na yeye ni mtu wa kwanza kumshauri autoe wimbo huo.

Wise anasema baada ya Ben Pol kuona ameupenda huo wimbo ndio akamwambia aufanyie jambo lakini kutokana na wimbo kuwa na dakika nyingi alikataa kufanya lolote lakini alilazimishwa na kuamua kufanya kile ambacho aliweza kukifanya kwa muda huo lakini alikuwa amepewa nafasi kubwa  yakuingiza mistari na alikaata kutokana na urefu wa ngoma yenyewe.

kwaupande mwingine Wise one amesemabaada yakutoka wimbo huo anashukuru wasanii wakubwa kama Jux na Vanessa kuonesha kuukubali uwezo wake na amepokea hongera nyingi kutoka kwa mashabiki wa muziki.

pamoja na hayo anamshukuru Ben Pol kwakumuweka kwenye wimbo huo ulio kuwa mkubwa kwa muda mfupi.

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages