#NgelangelaNews
inakuletea majina ya vijana 10 walio Fanya vitu mbalimbali nakufanikiwa
kuvuka mipaka ya Dodoma pamoja nakuutangaza mkoa wadodoma katika
nyanja mbalimbali yakijamii, Siasa, Michezo, burudani NK, pia
wanastahili kuwa mfano wakuigwa kwa mwaka huu 2018.
1. MH ANTHONY MAVUNDE ni mtumishi wa serikali na kiongozi wa umma upande wa kwanza ni Naibu Waziri wa kazi vijana na ajira lakini pia ni mbunge wa jimbo la Dodoma mjini, amekuwa ni moja ya kiongozi ambaye Mara kadhaa amekuwa akihamasisha maendeleo kwakiasi kikubwa kwa kuwashika mkono vijana na wanawake katika shughuli za ujasiriamali na michezo, miongoni mwa vitu alivyovifanya kwa mwaka 2017 ni pamoja na kuwapatia mashine 31 wajasiriamali wa mkoa wa Dodoma zitakazo wasaidia katika ufugaji nakukuza sekta ya viwanda, amekuwa kuvutio kwa vijana kutokana na jitihada zake za kuhamasisha michezo kutoa hamasa kwenye timu ya DFC, amefanikiwa kuupatia hadhi mchezo wa drafti, aliahidi kutengeneza studio, ya kurekodi nyimbo za wasanii pamoja na eneo la mazoezi kitu ambacho kitawapa nafuu vijana wenye vipaji.
2. #MC_PILIPILI ni mchekesha na ni mshehereshaji wa shughuli mbalimbali amekua akipiga hatua kila siku, huku akipeleka kazi Zake mpaka nje ya Tanzania, amefungua kampuni yake ya Pili pili event aliyoajiri vijana zaidi ya 10 nawengine wakitokea Dodoma, mwaka 2017 aliuza kitabu cha maisha yake kilichofanikiwa kuuza na alisambaza kote nchini, anamiliki YouTube channel yenye nguvu zaidi nchini, pia ni mchekeshaji ambaye amekuwa akitaja zaidi mahala alipotokea.
3. Moni Awadh Central ni msanii wa bongo fleva anaefanya Rap na Hip Hop mwaka 2017 ulikua wenye mafanikio zaidi kwake kwakutengeneza hit songs Kama *usimsashau mchizi*, *matango pori*, *tunaishi nao* na *bongo super star*, ni baadhi ya ngoma zilizo sikika zaidi hadi nje ya Dodoma, kwajitihada zake alizowekeza anafaa Kuwa msanii wakuigwa nakupewa heshima kutokana na kuipeleka mbele zaidi nakuitangaza Dodoma.
4 #NICKLASS ni muongozaji wa video za muziki namatukio mbalimbali kutoka Dodoma kwasasa makazi yake ni Dar es salaam amefanya video kubwa za wasanii wa bongo fleva nchini kama Feza Kessy, Roma, Moni Centralzone, NK. wapo vijana wengine wanahitaji kufanya kazi kama zake ni bora wakaiga mfano wake wakutokukata Tamaa.
5. #BIN_LADEN ni mtayarishaji wa muziki aliyepata umaarufu mkubwa mwaka huu baada ya lile tukio lakutekwa, lakini hakurudi nyuma aliendelee kuweka jitiada kwny ubunifu wa kazi zake nyimbo alizotengeza nyingi zinanembo ya jina lake, amefanyakazi na msanii kama Moni, Roma, stamina, Young killer, Cyril kamikaze NK, kupitia yeye amesababisha jina ladodoma likitajwa mara kwa Mara kwenye vyombo vya habari mbalimbali.
6. Laurent Mkombozi ni mwanamitindo na mbunifu wa mavazi kutoka kampuni yake ya mkombozi design, ametengeneza nakubuni nguo zake aina za suti nakuwavalisha watu maarufu Kama wasanii, viongozi NK, amehudhuria kwenye matamasha mbalimbali ya mavazi nje ya Dodoma, anastahili kupata heshima kutokana na kazi anayoifanya kwa mkoa wadodoma kutofanywa na vijana wengi.
7. #DJ_BARSER ni dj toka mkoani Dodoma amefanikiwa kufunga mwaka Kwa kishindo kikubwa baada yakushiriki shindano la Sminorff dj search nakuibuka mshindi kwa kanda ya kati nakufanikiwa kufika kushindana level ya kitaifa nakuibuka mshindi namba mbili, anaingia kwenye orodha hii kwajitiada zake zakutokukata Tamaa Kwan ameshindana mara nyingi bila kushinda nahakukata tamaa, Kwa mwaka 2017 ameitangaza Dodoma kwani dodoma imefanikiwa kutoa mshindi wa sminorff dj search. Anatufundisha kutokukata Tamaa.
8. Eng Msofe ni graphic designer aliefanya cover za wasanii mbalimbali, cover za matukio ya burudani pamoja na biashara mbalimbali,mvuto wa cover zake umefanya watu wengi kutamani kuwa kama yeye hususani katika utengenezaji wa cover, amefanya kazi kibao za wasanii wadodoma na nje yadodoma lakini pia amefanya kazi na viongozi wa umma,vyombo vya habari na NK, wengi wamekuwa wakimtaja Kama mtu wamfano hususani vijana wanaohitaji kufanya kazi kama zake.
9. ABOUE MFAUME & ARON LUHAMBO wote ni wachezaji wa mpira wakitokea Dodoma nawamepata nafasi yakusajiliwa na timu zinazo cheza ligi kuu, Abou akiwa ni mchezaji wa mbao FC, na Aron ni mchezaji wa Stand united kwa mwaka huu wamefanikiwa kutajwa mara nyingi kwenye vyombo vya habari.
10. Ally Gonta nikijana ambae hajachukuliwa kwa ukubwa ndani ya Dodoma lakini ni moja ya watu walioweza kuipa hadhi Dodoma kwakutengeneza nembo ambayo imekuwa ikutumiwa na wanadodoma wote walio ndani ya Dodoma na nje ya Dodoma ambayo imekuwa printed kwenye T-shirt na masweta kwakuandika T255DOM huwezi pinga kuwa hii ni logo yenye nguvu ambayo inaitambulisha dodoma, walioweza kuipa nafasi ni pamoja na Mh mbunge wa Dodoma Anthony Mavunde, kwa 2018 ni vyema kijana huyu akapewa nafasi yakuonesha alichonacho zaidi kwani anaweza akawa ni mbunifu wakuigwa na vijana wengi zaidi nakuongeza idadi ya vijana waliojiajiri.
NB: IMEANDALIWA kwakuzingatia zaidi wale vijana wanao Fanya harakati zao ndani ya Dodoma ama walio Hama mkoa baada ya kupiga hatua kikazi kutokana na kutafuta nafasi zadi.
Nini maoni yako.
@ngelangelanews.blogspot.co