MAKALA:SALAM KWA DOGO JANJA KWA HII VITA CHUKUA GWARA. - NGELANGELA NEWS

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday, July 14, 2017

MAKALA:SALAM KWA DOGO JANJA KWA HII VITA CHUKUA GWARA.


Katikati ya mwaka 2017 na ukiwa ni msimu wa baridi kwa maeneo mengi bongo,mara baada ya shughuli zangu za kila siku nafungua simu yangu na kuingia kwenye mitandao ya kijamii kupata habari mbalimbali.Ndipo nakutana na chapisho kutoka kwenye page moja kubwa katika mitandao ya kijamii.
 Image result for dogo janja
chapisho hilo ambalo lilileta mzozo mkubwa kwa wachangiaji waliokuwa wakijadiri wachache wakikubaliana na wengi walipinga.Chapisho hilo lilikuwa na andiko lililosomeka je? ,Dogo janja ndie msanii anaevaa vizuri kuliko wote?. Baadhi ya wachangiaji waliandika Huyo dogo amechanganyikiwa kwenye swala la kuvaa unamuacha vipi Simba, Diamond Platnum ,Jux au Bayser Mr. Blue dogo bado sana kwenye kuvaa na wengine wakichangia dogo kweli anavaa ila sio mkali kuliko wote.

Kama masihara vile issue hio ilivuma na kuzidi kuwa kubwa na kupata nafasi kubwa katika mitandao yote ya kijamii,haikuishia hapo mpaka vituo vya radio na TV vililizungumzia hii issue,hususani pale mkali kutoka lebo ya PKP Nedy music aliposema Dogo janja anazeeka vibaya na uwezo wake wa kufikiri unapungua kila siku,na kuhusu kuvaa Dogo janja kafundishwa na madee hawezi kushindana na mimi labda ashindane na densa wangu alisikika Nedy music.

Kwa yoyote anayekumbuka hii issue ilikuwa kubwa sana na takribani majuma mawili jina la Dogo janja lilikuwa kwenye chati ya juu mno.kabla issue haijapoa,siku moja mida ya jioni nikiwa kwenye daladala nasikia nyimbo mpya ya Dogo janja ikitambulishwa, nyimbo hio mtangazaji anasema inaitwa ukivaaje unapendeza.


Niliposikiliza mashairi ya nyimbo hio nikajikuta nikicheka na kusema mwenyewe dah! huyu dogo mbunifu sana ,nikikumbuka siku chache alivyotengeneza kick kabla hajatoa nyimbo hii ambayo anazungumzia jinsi anavyojua kuvaa na akivaa vipi anapendeza na kwenye chorus akituuliza ukivaaje unapendeza.Nakupa gwara Dogo janja na menejimenti yako kwa ubunifu mliotumia kutaka ngoma yenu isigoee,mngeweza kuwatafuta amber lulu au Gigy money akawashika makalio au hata kupakwa mafuta kama Ben paul ,lakini mlikaa chini na kubuni kitu cha tofauti tena kisicho na ukakasi wowote .Chukua gwara Dogo najua ukivaa vyovyote unapendeza tu au sio hata ukivaa suti ya turubai na tishert ya hakatwi mtu hapa 

Tukutane Jumatatu na ijumaa tamu chungu segment ndani ya micharazo time yaDodoma Redio saa kumi na moja kwa audio ya makala kama hii na nyinginezo nyingi
imeandikwa na Daniel Mihanjo Wa Pili

SOURCE DODOMA FM RADIO.

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages