MAOMBI 6 MAALUMU TOKA HALMASHAURI YA DODOMA MOJAWAPO NI DODOMA KUWA JIJI. - NGELANGELA NEWS

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday, July 13, 2017

MAOMBI 6 MAALUMU TOKA HALMASHAURI YA DODOMA MOJAWAPO NI DODOMA KUWA JIJI.

Siku ya 11 tarh july 2017 halmashauri ya manispaa ya Dodoma iliwasilisha taarifa ya manispaa kwa waziri wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi Mh George SimbaChawene ripoti hiyo ikujumuisha utendaji wa halmashauri tangu mamlaka ya ustawishaji wa makao makuu (CDA) kufutwa na kuagiza shughuli zote zifanywe na halmashauri ya manispaa ya Dodoma.



Image result for dodoma
Katika taarifa hiyo Halmashauri ya manispaa ya Dodoma ilitoa mapendekezo yake maalumu, Ambayo ni.

1.Kwa kuwa halmashauri ya manispaa ya dodoma imekidhi vigezo vya kuwa jiji nataratibu za kupitisha mapendekezo katika kamati ya ushauri ya wilaya (DDC) na kamati ya ushauri ya mkoa (RCC) zimekamilika, kwa sasa mapendekezo hayo yamewasilishwa TAMISEMI, Tunaomba halmashauri ya manispaa ya Dodoma iweze kupandishwa hadhi na kuwa jiji kwa kuzingatia sasa makao makuu yamekwisha hamia Dodoma.

2.halmashauri ya manispaa ya Dodoma imepokea watumishi 136 wa kada mbalimbali kutoka kwa iliyokuwa CDA kimsingi idadi ya watumishi wa manispaa ya Dodoma kwenye idara mipango niji na ardhi ni ndogo ukilinganisha na mahitaji hivyo halmashauri inaomba kuongezewa wataalamu.

3 kufuatia agizo la mh Waziri mkuu ofisi ya mamlaka ya ustawishaji makao makuu CDA iwe kutuo kimoja cha kutoa huduma ya ardhi  (one stop central) halmashauri ya manispaa ya dodoma imekwisha tenga ofisi kwaajili ya kamishina msaidizi ili kuweza kutoa huduma kwa urahisi. Tunaomba wizara ya ardhi iweze kuwaleteta maafisa hao ambao kimsingi watahusika na uidhinishaji na usajili wa hati kwa halmashauri ya manispaa ya Dodoma tu. hasa ukizingatia halmashauri ya manispaa ya dodoma inashughulikia uendelezaji makao makuu ya nchi na kutoa huduma za kijamii kama halmashauri zingine nchini.

4 halmashauri ya manispaa ya dodoma inaomba kupokea na kutuma Tozo mbalimbali za ardhi ambazo zilikuwa zikipokelewa na iliyokuwa mamlaka ya ustawishaji makao makuu CDA ili kuweza kukidhi mahitaji ya kutekeleza miradi na upimaji wa viwanja ujenzi na ukarabati wa nyumba.

5 halmashauri ya manispaa ya dodoma inaomba kupatiwa fedha kupitia mfuko wa viwanja wa wizara ya ardhi plots development revolving fund (PDRF) ili kuwezesha upimaji wa viwanja ufanyike kwa haraka.

6 halmashauri ya manispaa ya dodoma inaomba kuruhusiwa kutumia fedha kwenye akaunti za iliyokuwa mamlaka yaa ustawishaji makao makuu ili kuendeleza miradi ambayo ilikuwa inaendelea ya upimaji wa viwanja, ukarabati wa nyumba na ufunguaji wa barabara.


Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages