SHILOLE AWACHANA WASANII WANAO SHOOT VIDEO ZA NYIMBO ZAO NJE YA TANZANIA - NGELANGELA NEWS

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Sunday, June 4, 2017

SHILOLE AWACHANA WASANII WANAO SHOOT VIDEO ZA NYIMBO ZAO NJE YA TANZANIA

Kutokana na wasanii wengi nchini kutokuwa na uzalendo wa nchi yao imetajwa kuwa ni sababu mojawapo inaypolekea kutoka nje ya Tanzania kwa ajili ya kushoot video za nyimbo zao.

Akizungumza na kipindi cha micharazo time ya Dodoma fm radio Shishi Trump’ maarufu kama shilole amesema kitendo cha baadhi ya wasanii  kuwa na utaratibu wa kwenda kushoot video zao nje ya Tanzania ni kukosa uzalendo na nchi yao.

Shilole amesema kutokana na chance ambayo ameipata kutembea mikoa mbalimbali nchini kutokana na kazi yake ya mziki amegundua mikoani kuna location nzuri kwa ajili ya kushoot video kuliko hata nje ya Tanzania.

‘’Unajua kabala sijapata nafasi ya kutembelea kwenda mikoa mbalimbali nchini kama mwanza,Morogoro na mikoa mingine sikujua kama mikoani kuna location nzuri hivi lakini sasa tatizo lipo kwa wasanii wanakimbilia kushoot nje kuliko hata kusapoti location za hapa hapa’’Alisema shilole

Shilole amehaidi kazi mpya kwa mashabiki wake baada ya mwezi mtukufu wa ramadhani hivyo wakae mkao wa kula kutoka kwa Shish Trump

Story na  Beny  Bert                    


Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages