Akizungumza na kipindi cha micharazo time ya Dodoma fm radio amesema hamna msanii aliyezaliwa anajua kuongea kingereza hivyo kama wana mshangaa na yeye anawashangaa.
Pia amesema kuna wasanii wengi na wakubwa nchini wamejifunza lugha hiyo wakiwa wanajulikana kimataifa huku akimtaja Diamond platnumz kama miongoni mwao pamoja na alikiba.
‘’Nawashangaa sana wasanii wanaoniambia sijui kuongea kingereza wakati utakuta hata wenyewe hawajui!!!! Hakuna mtu alizaliwa anajua kuongea lugha hiyo isipokuwa kuna hatua ambazo unajifunza ndipo unajuaa mbona Diamond alikuwa hajui chochote na yeye alikuwa kama mimi tu ukimzungumzia alikiba nay eye amejua baada ya kutambulika kimataifaa so tusichekane na wala tusichukuliane powa hamna kisichowezekana usishangae kuona mwakana harmorapa anaongea kingereza kama cha Jay z’’Alisema Harmorapa
Alipoulizwa kuhusu kazi zake za mziki ambazo zipo ndani na hajazitoa mpaka sasa hivi amesema ana truck tano hivi anasubiri muda tu uje alfu aachie.
Harmorapa bado anafanya vizuri na wimbo wake Nundu alio mshirikisha mkali CPWAA na Ronei ambaye ni msanii mpya kwenye lebo ya SABUKA MUSIC.
Story na Beny Bert Chanzo Micharazo time Dodoma fm