Mwanadada huyo ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na kipindi cha micharazo time cha Dodoma fm radio ambapo amesema kuwa amefurahi kupata nafasi ya kuingia msimu wa Coke studio nchini Kenya 2017 hivyo anaamini ni hatua moja kubwa japo hakuwai kufikiria.
Akizungumzia kuhusu kuhusu experience au uzoefu alioupata coke studio amesema amejifunza jinsi wasanii wa nchi mbali mbali wanavyo fanya kazi zao pamoja na kujali mda.
‘’Unajua ndo mara yangu ya kwanza mimi kuingia Coke studio na sio ishu ndogo ukizungumzia Coke studio ni Dunia unaizungumzia so ni ktu ambacho sikufikiria kama ntakuja siku moja nikutane na wasanii wakubwa kutoka Zimbabwe,Malawi,Nigeria na sehemu zingine kwahiyo nawaambia vijana wenzangu ni mwiko kukata tamaaa kwa sababu hujui kesho yako, kiukweli mi nime hustle miaka mitano lakini sikukata tama na leo hii nimeanza kuona matunda’’Alisema Nandy
Katika hatua nyingine mwanadada huyo amesema ana kazi yake mpya japo hajaweka wazi amefanya na msanii gani nchini.
Hata hivyo bado anafanya vizuri na wimbo wake unaoitwa one Day
Story na Beny Bert Chanzo Micharazo time