CHONDE CHONDE MTOTO CHUKUA VYOTE KWANGU ILA RANGI CHUKUA KWA MAMA AKO NKAVIMBE KWA WAMAKONDE MTWARA''HARMONIZEE - NGELANGELA NEWS

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Sunday, June 4, 2017

CHONDE CHONDE MTOTO CHUKUA VYOTE KWANGU ILA RANGI CHUKUA KWA MAMA AKO NKAVIMBE KWA WAMAKONDE MTWARA''HARMONIZEE

Baada ya kuachana na mrembo wa filamu Tanzania Jacqueline Wolper, muimbaji wa  wimbo  NIAMBIE kutoka WCB, Harmonize, ameonesha picha ya mpenzi wake mpya mzungu pamoja na kuthibitisha ni mjamzito.

Muimbaji huyo ambaye alikuwa kimya kuzungumzia mahusiano yake mapya na mzungu huyo licha ya kuzungumzwa na watu kwenye mitandao ya kijamii, Jumapili hii ameonyesha vipimo vya Ultrasound vikionesha mpenzi wake huyo mzungu ni mjamzito.


“Mnh! nawaza huu mchanganyiko wa damu ya kimakonde na ya kizungu sijui itatuletea mwana gani… asa nikiona kakomwe hapo, kananistua😁…Chonde mtoto chukua vyote kwangu ila kwenye rangi jitahidi uibe ya mama yako…..!!! nikavimbe Mtwara 😊,” aliandika Harmonize Instagram.

Hata hivyo muimbaji huyo hakuweka wazi ujauzito huo ni wa miezi mingapi.

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages