Tukio la kutekwa kwa wasanii hao kutoka tongwe records lilihusisha wenzake 2 ambaye ni producer Binladen,Pamoja na Roma.
Akizungumza na micharazo Time ya Dodoma fm radio amesema alikuwa anakaribia kukamilisha album hiyo lakini bahati mbaya akajikuta wametekwa na watu wasiojulikana hali iliyopelekea kukwamisha kwa albam hiyo.
‘’Unajua nilifika hatua ya mwisho ya kukamilisha albam hiyo lakini ghafla tukajikuta mikononi mwa watu wasiojulikana na ndo walio pelekea nishindwe kumalizia albam yangu’’Alisema Moni central zone
Ameongeza kuwa tayari ameongea na wasambazaji wa albamu ili akiitoa iweze kusambaa kwa mashabiki wake wote.
Moni Centroozone anafanya vizuri na wimbo wake Tunaishi nao,
Na Beny Bert Chanzo micharazo time