Msanii wa mziki wa kizazi kipya Azma Mponda kutoka jiji la
mbeya amethibitisha kuanza kuona mafanikio ya muziki wake baada ya kuachia
kazi yake inayoitwa ASTARAVASTE aliyo
mshirikisha belle 9 ambayo aliiachia mwishoni mwa mwaka jana.
Akizungumza na Micharazo time ya Dodoma fm radio amesema baada
ya kuachia kazi hiyo imemfanya aongeze fan base wengi tofauti na mwanzo ambapo alikuwa hajulikani.
Kutokana na kuongezeka kwa wasanii wapya kila kukicha ambapo
imekuwa changamoto kwa baadhi ya wasanii akiwepo Mo music na kudai ilimlazimu
kukaa kimya na kutathmini jinsi gani atarudi kwenye mziki lakini kwa upande wa
Azma imekuwa tofauti huku akidai wasanii wapya hawamuumizi kichwa isipokuwa
kikubwa ni Connection ya kujuana na watu wengi.
‘’Unajua katika hii
game yetu ya mziki ndio kuna wasanii wengi lakini kikubwa uwe na connection tu
hapo inakuwa rahisi sana ya kujuana na watu ili uweze kujulikana kila sehemu’’Alisema
Azma
Ameongeza kuwa kiki inaweza ikapelekea msanii kushuka au
kupanda kimziki ukitofautisha na msanii ambaye ametoka kwa nguvu zake mwenyewe
binafsi kimziki.
Azma anafanya vizuri na wimbo wake Garagasha alio
mshirikisha Joseph Mbilinyi maarufu kama sugu pamoja na Izzo bissnes wote kutoka katika jiji la Mbeya