Serikali imetakiwa kuhakikisha inakuwa karibu na wakulima
wamatikiti pamoja na kupanga bei elikezi ambayo itakuwa na manufaa kwa wakulima
na walanguzi.
![]() |
imma sadala mkulima wa matikiti |
hayo yamezungumzwa na mmoja wa wakulima wa zao hilo Bw
Emanuel Sadala kutoka kijiji cha mvumi mkoani Dodoma na kusema wamekuwa
wakipata changamoto yakupangiwa bei na madalali wa zao hilo hali inayo pelekea
kuto nufaika na zao hilo.
Pamoja na hayo amesema wakulima wa matikiti mkoani Dodoma
wamekuwa wakipata changamoto ya kununua dawa za mazao kwa bei kubwa pamoja na
kukosa maduka makubwa ambayo yanauza dawa na hupelekea kuzifuta mikoa mingine
jambo linalo sababisha kupoteza muda.
Sanjari na hayo ameiomba serikali kuhakikisha inafungua
viwanda na kuruhusu wawekezaji kuwekeza kwenye sekta hilo ili iwe rahisi kwa
wakulima kupeleka mazao mbalimbali pamoja na kuongeza wigo wa mauzo.
Na Benedict Ngelangela.