![]() |
moni centralzone |
Sasa kupitia kipindi cha micharazo time kinachoruka 98.4 Dodoma fm radio nakuongozwa na Benedict Ngelangela alisikika msanii Moni Centralzone akielezea ni jinsi gani LANGA aliweza kumsaidia na kumuonesha njia zakupitia kwenye muziki na vitu vya muhimu vya kufanya ili aweze kufanikiwa.
Moni amevitaja vitu ambavyo hawezi kuvisahau kwa LANGA moja wapo ni kuwa na imani ya vitu ambavyo unafanya kwani langa alikuwa anaamini kuwa ukifanya kitu kwa ubora lazima utayaona mafanikio, pia amesema Langa hakuwa mtu wakakata tamaa kwenye kazi zake alikuwa ni mpambanaji wa kweli.
Pamoja na hayo Moni amesema hatasahau siku ambayo Langa alimwambia kuwa ipo siku atakuwa ni msanii mkubwa kutokana na uwezo wake wakuandika mistari na alikuwa ni mtu pekee alikuwa akiwatafutia connection kwa baadhi ya wadau.
