MBUNGE WA DODOMA MJINI ANTHONY MAVUNDE AKUTANA NA BALOZI WA USWIZI, UFADHILI WA SH 34,000,000 USD KUTOLEWA KWAAJILI YA VIJANA. - NGELANGELA NEWS

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday, June 12, 2017

MBUNGE WA DODOMA MJINI ANTHONY MAVUNDE AKUTANA NA BALOZI WA USWIZI, UFADHILI WA SH 34,000,000 USD KUTOLEWA KWAAJILI YA VIJANA.

Leo asubuhi nimefanya mazungumzo na Balozi wa Uswisi Mh Florence Mattli katika ofisi za Wizara ya Kazi,Vijana,Ajira na Watu wenye Ulemavu-Dodoma juu ya namna bora ya ushirikiano kati ya Tanzania na Uswisi katika eneo la Ukuzaji Ujuzi kwa Vijana kupitia mpango unaotekelezwa na Wizara.
Image may contain: 2 people, people sitting
ANTHONY MAVUNDE KUSHOTO AKIWA BALOZI WA USWIZ

Balozi Mattli ameupongeza mpango wa Wizara wa utekelezaji wa Program ya Ukuzaji Ujuzi kwa Vijana nchini kupitia mafunzo stadi ambayo yana lengo la kuwajengea Vijana wa Tanzania ujuzi stahiki na hivyo kuwawezesha kuwa na sifa za kuajiriwa,Kujiajiri na kuajiri Vijana wengine.

Balozi Mattli ameahidi kushirikiana na Serikali katika kuunga mkono juhudi za Wizara katika uendeshaji wa Mafunzo ya Ufundi kwa Vijana kwa kufadhili kiasi cha Shilingi 34,000,000 USD kwa miaka 12 kwa ajili ya utekelezaji bora wa Mpango wa Ukuzaji Ujuzi kwa Vijana nchini.
 Image may contain: 3 people, people smiling, people sitting


Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages