Msanii wa
mziki miondoko ya hip hop nchini mansuli amesema kutokana na msanii mwenzake
anayeunda kundi la capital letter anayefahamika kama Veri kukabiliwa na
majukumu imepelekea yeye kuendelea
kulinda jina la kundi hilo ili lisipotee kwa mashabiki wao.
Akizungumza
na mtangazaji wa kipindi cha micharazo time kinachoruka kupitia Dodoma redio
msanii huyo amesema baada ya veri ambaye ni msanii anayeunda kundi la Capital
letter kuoa hajawa serious katika muziki.
Mansulii
amesema mara nyingi amekuwa akimlazimisha kufanya project nyingi katika kundi
hilo ili kuendelea kulinda jina la kundi hilo na kuepusha kupotea kwa
mashabiki,
‘’Unajua mara nyingi
sana tikitoa kazi ya kundi la capital letter inaonekana kama kazi yangu binafsi
hiyo ni kutokana na msanii mwenzangu kuwa bize sana na majukumu yake ya
familia na sasa hivi ameoa kwahiyo hata kwenye media tour za mikoani kwenda
kutambulisha nyimbo zetu mimi ndo ambaye
naenda‘’alisema mansuli
Ameongeza
kuwa Capital letter inajihusisha na na vitu vingi ikiwepo masuala ya ulinzi na
vitu vingine.
Capital
letter sasa hivi wanafanya vizuri na wimbo wao TUSTAREHE ambao wamemshirikisha
chege
Na Beny
Bert
Social
network Beny Bert