Msanii wa mziki wa bongo fleva kutoka Dodoma amesema kuna
utofauti mkubwa kwa msanii ambaye anafanya mziki wake akiwa Dodoma na Yule
anaye fanya mziki akiwa Dar es salaam.
Akizungumza na Beny Bert mtangazaji wa kipindi cha micharazo time kinachorushwa na
Dodoma fm msanii huyo amethibitisha kweli kuna utofauti mkubwa kwa msanii
ambaye anafanya mziki akiwa Dodoma ukilinganisha na Yule ambaye yupo Dar es
salaam.
Wise one amesema ukiwa Dodoma hata kama una nyimbo mbili
unajiona kwamba wewe ni msanii na unajua mziki zaidi ya wenzako na ni vigumu
kukutana na changamoto zitazo kufanya ujifunze vitu vingi zaidi katika tasnia
ya mziki.
‘’Unajua
Dodoma ukiwa pale una vimba mtaani unajiona wewe ndo wewe kiasi kwamba hamna
anayeweza kuwa zaidi yako lakini ukiwa Dar kwanza hata kama una nyimbo tatu
unajiona bado kwahiyoo unakomaaa ili uwafikie’’Alisema wise one
Kutokana na ukaribu alinao wise one na msanii wa miondoko ya
RNB Ben pol amesema amepata connection
nyingi ikiwepo ya kufanikisha kufanya nyimbo na mr,Eazy kutokea nigeria pamoja
na Eddy Kenzo wa Ugandaa.
Social network Beny Bert