HUWEZI KUFANIKIWA BILA KWENDA KWA MGANGA''MENEJA MANENO - NGELANGELA NEWS

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wednesday, May 31, 2017

HUWEZI KUFANIKIWA BILA KWENDA KWA MGANGA''MENEJA MANENO

Aliyekuwa meneja wa Diamond platnumz,Rich mavoko pamoja na samu wa ukweli Meneja maneno amesema katika kazi yoyote huwezi kufanikiwa bila kwenda kwa mganga.

Akizungumza na mtangazaji wa kipindi cha micharazo time kinacho ruka kupitia Dodoma fm radio  Beny Bert meneja asema katika kazi yoyote huwezi kufanikiwa bila kwenda kwa mganga kutokana na kila mtu anavyo amini na imani yake.

Amesema kipindi alipokuwa meneja wa Diamond,Rich mavoko na samu wa ukweli  amekiri wamewahi kwenda kwa waganga mara kibao wakiamini wanafanikiwa.

‘’Unajua hapa duniani huwezi kufanikiwa bila kwenda kwa mganga hayo yote ni kutokana na mtu imani aliyonayo hata mimi naenda kwa mganga ili niweze kufanikishaa’’alisema meneja maneno



Sasa hivi meneja maneno anafanya vizuri na wimbo wake jasho lake alio mshirikisha Dullysks

Na Beny Bert 
  
Social network  Beny Bert                           

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages