Kutokana na mwingiliano kazi kati ya director na
mwanamziki wa hip hop kutoka Dodoma Bujanlau the king imepeleke
kuchelewesha kuachia kazi mpya ya msanii
huyoambayo inaitwa PRESHA.
Rapa huyo aliyasema hayo wakati akizungumza na kipindi cha
micharazo time cha Dodoma fm radio ambapo amesema ananyimbo tano ambazo
amerekod toka mwezi wa kwanza lakini akaona bora aachie wimbo huo kutokana na
kuwepo kwa presha ya mambo mengi kipindi hiki ikiwepo siasa,uchumi,muziki nk.
Akijibu swali la matumizi ya mitandao ya kijamii kwa upande
wake amesema alipoona Director wa video hiyo akaamua aendelee kupromote katika
mitandaao ya kijamii ili kuwaweka mashabiki mkao wa kula ambapo amehaidi kabla
ya mwezi ramadhani atakuwa ameachia kazi hiyo.
‘’Mara nyingi
mimi mitandao yangu ya kijamii huwa natumia vizuri hasa nahakikisha na promote
kazi zangu ili ni push harakati zangu kwahiyo huwezi kunikuta na post ujinga
ujingaa’’Alisema Bujanlau
Kwa sasa hivi mwanamziki huyo yupo Dar es salaam anasubiri
muda ufike afanye collable na waheshimiwa kutoka bungeni japo hajaweka wazi
kama ni mh.Joseph mbilinyi maarufu kama sugu au Joseph haule ambaye na mbunge
wa mikumi professor jay