JIMMY YEYOO - WASANII WADODOMA HAWATAENDELEA KWASABABU NI WANAFKI. - NGELANGELA NEWS

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday, March 10, 2017

JIMMY YEYOO - WASANII WADODOMA HAWATAENDELEA KWASABABU NI WANAFKI.

Msanii wa hip hop mkoani Dodoma wakuitwa JIMMY YEYOO ambaye hivi karibuni ameachia wimbo wake unaitwa Stick with me alio mshirikisha GIFTED SON amesema moja ya mambo ambayo yanaididmiza sanaa ya Dodoma ni unafiki toka kwa wasanii.
 Image may contain: one or more people, people standing and closeup
JIMMY amesema wasanii wengi wa dodoma hawana upendo toka kwa wasanii wenzao na wamekuwa wakiwatengenezea fitina wasanii wengine wasisikike kwenye radio au pia kuwanyima watu wengine wasipewe fursa za show nakuamini wao pekee ndio wanao takiwa kusikika pekee nakuonekana.

pia ameongeza nakusema kuna wasanii ambao wamekuwa kipaumbele kuomba msaada kwasanii wengine kupostiwa kava zao lakini zikija zawenzao hawaoneshi ushirikiano hata kidogo na mwisho wa siku page zao zinajaa kazi zao na picha zao pekee.

aidha amedai kuwa hajawah kuwa na tatizo lolote na msanii wa dodoma ila anaamini wapo baadhi ambao hawapendi kile ambacho anakifanya.

@source micharazo time ya 98.4 Dodoma fm radio.

Na Benedict Ngelangela.


Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages