
akizungumza na mtangazaji wa kipindi cha micharazo time toka 98.4 Dodoma fm radio kinachoongozwa na Benedict Ngelangela BEN POL amesema wapo baadhi ya wasanii ambao huwa anawasikiliza lakini wengine wamekuwa wakimvutia na wengine wakiongeza juhudi watakuwa vizuri zaidi.
BEN POL amemtaja msanii wakuitwa WISE ONE kuwa ni moja ya wasanii ambao anawakubali kwasasa na tayari wamesha fanya nae kazi pia ameamua kumchukua WISE kama mdogo wake na huwa wanatembeananae hadi kwenye show zake.
Pia kwa upande mwingine BEN POL ameongoza kwa kumtaja msanii wa kike wakuitwa KOKU nakusema anauwezo mkubwa na akikaza atafika mbali.
pamoja na huyo BEN POL amemtaja ONESIX kam msanii anae mkubali na anauwezo mkubwa sana.
Kwasasa BEN POL anatamba na wimbo wake PHONE