wakiongozwa na mkurugenzi wa BIORN amesema MOH waliweza kufikisha mambo matatu makubwa ambyao wangetamani kuona yanafanyiwa kazi ndani ya sanaa yetu ndani ya mkoa wa dodoma ili sanaa hii iweze kufika mbali zaidi nakutambulika zaidi.
pamoja na mambo ambayo yaliwasilishwa kwa Mh mbunge ni pamoja na kuhakiksha wasanii wa Dodoma wanatumika kama brand kwenye makampuni ambayo yanafanya kazi ndani ya mkoa wa Dodoma, pia kuhakikisha wasanii wadogo wanapata nafasi ya kukutana na wadau wakubwa wa muziki nchini pamoja na kupanua kazi zao kusikika mbali zaidi.
Baada ya kuyapokea hayo Mh mavunde alipata nafasi ya kuzungumza na waliohudhulia kwenye kikao hicho nakusema miongoni mwa vitu ambavyo anatamani kuona ndani ya Dodoma ni kuona Dodoma inakuwa kisanaa na ni miongoni mwa vitu ambavyo ameviwekea kipaombele na tayari ameanza kuvifanyia kazi kwakuunda umoja wa wasanii ambao ni DODOMA KWANZA.;
Aidha amesema kuanzia sasa mtendaji mkuu wa Dom kwanza utaongozwa na yeye mwenyewe ili kupunguza baadhi ya malalamiko yaliyojitokeza mwaka uliopita na tayari ameanza ujenzi wa ofisi ambao unakaribia kukamilika kwani upo kwenye ngazi ya mwisho huko ofisi hiyo ikiambatana na ukumbi mkubwa utakao kuwa ukiwakutanasha wasanii mbalimbali kwaajili ya mazoezi.
pamoja na hayo Mh Mavunde amewataka wasanii wa dodoma kuhakikisha wanabadilika na kuwa wakisasa zaidi ili iwe rahisi wao kusaidiwa kirahisi, "nilazima msanii aonekane vizuri hususani kimuonekano jitambulisho kama msanii ili hata mtu akikuona ajue kuwa wewe kweli ni msanii kuvaa vizuri haijalishi lazima uvae mregezo ushushe suruali hapana nilazima ujitengeneze vizuri uwe msafi na tabia nzuri pia" alisema mh Anthony Mavunde.