Najua kuwa wajua kuwa wapo watu ndani ya mkoa wa Dodoma wanasapoti sana wasanii wanao chipukia kwa hali ya juu na kwenye list yao huwezi acha kumtaja blogger Mkamanga kutokana na jitiada zake za kudeal na wasanii.
Mkamanga ni moja ya watu ambao kipindi cha nyuma walikua karibu sana na Msanii wa muziki ambae anashikiria tuzo ya Msanii bora wa kiume kupitia tuzo za Nyambogo Awards.
Lakini hivi karibuni imetokea tafarani ya hali ya juu ambayo imewashtua watu wengi na kushindwa kuamini kama vijana hao hawapo katika mahusiano mazuri.
Kupitia group LA wasanii LA whatsap linaloitwa Jukwaa la wasanii, Jacco Beat ali anza kwa kuandika maneno ya kumtaka mkamanga kuondoa video yake kwenye blog yake ya mkamanga.com kitu ambacho kilimkasirisha mwanaharakati huyo ndipo alipo anza kujibu mashambulizi ya hali ya juu nakumuuliza Jacco kwanini aliomba aiweke kwenye blogg halafu anasema itoke tena kitu ambacho Mkamanga aliona kama dharau kutoka kwa msanij huyo.
Haikuishia hapo Jacco nae aliendelea kujitutumua kwakung'ang'ana kuwa video iyo itoke, mkamanga na Jacco wakaendelea kujibishana ndipo tulipo anza kujua tusiyoyajua japo hakuna aliyethibitisha hayo mambo.
Mkamanga anamtuhumu Jacco beat kuwa ni mchawi na anawaroga wasanij wake wenzake wa Dodoma pamoja nakutengeneza fitina za hali ya juu ili wasimzidi.
Pia Mkamanga amemtuhumu Jacco Beat kuwa amemroga Kimambo amekimbia mji na kumuachia studio.
Mkamanga anasema yeye ndiye alie muomba Backamaza amtengenezee studio yake ya kwanza lakini hajui kwanini hataki kumuheshimu na anazifi kumdharau kila siku, na hicho ndicho ambacho.kimemkwaza Mkamanga.
SOMA SCREENSHOTS TOKA GROUP HILO LA WHATSAP.