Mchekeshaji na Mc kutoka ndani ya mkoa wa mkoa wa Dodoma ambae pia anashikiria tuzo ya Mc bora wa mwaka 2016 kupitia tuzo za Insta Awards amewataka ma Mcs wanao chipukia kuto ogopa ushindani kutokana na kuongezeka kwa ma Mc kibao ndani ya nchi ya Tanzania.

Mc Pilipili ameyaongea hayo kwenye mahojiano na kipindi cha Africa Moto kinachoongozwa na Josephine Kaponya kutoka 98.4 Dodoma fm radio, pia ameongeza kwa kusema kila mtu anaye hitaji kufanikiwa lazima afanye kazi kwa bidii pamoja na kuwa mbunifu kwa hali na mali.
Mc pili pili anatarajia kufanya show ya shukrani ndani ya Dodoma rayol village Siku ya tarehe 25.