Mwaka 2016 ulikuwa ni mwaka wenye harakati nyingi sana kisanaa na ndio mwaka ambao wasanii waliamini kuwa unaweza ukawa ndio mwaka wa Neema kwao baada ya kumpata Mbunge kijana na anayependa burudani pia aliahidi kuwasaidia vijana hao wenye vipaji.
Mh Anthony Mavunde kupitia dhamira yake ya kuwasaidia wasanii haikuishia kwenye kampeni tu bali mpaka ameshika madaraka bado alikuwa akikutana mara kwa mara na wasanii hao amboa mpaka sasa wanakiri kuwa hakuna kitu ambacho wamefaidika nacho tangu iteuliwe kamati ya kuwasaidia wasanii ambayo ipo chini ya Mh Anthony Mavunde mbunge wa mkoa wa dodoma.
Nimefanikiwa kupata ujumbe toka kwa mmoja ya msanii mwenye nguvu kubwa ndani ya mkoa wa dodoma akizungumzia hali ilivyo kwasasa kisanaa na pia nini kipo nyuma ya pazia.
Msanii huyu kwasasa anatamba na wimbo wake wa nimependa tena alioimna na msanii mwenzake WiseOne, ametuma ujumbe huu kwa Mh Anthony Mavunde.
SOMA HAPA CHINI.
######Tukiwa tunaumaliza mwaka ...nashukuru kupata nafasi hii nyingine tena nakushuru kila alieonyesha nguvu kunisapoti pia nishukuru sana wadau wa dodoma waliosapoti mziki kwa nguvu zote bila kuwasahau MAISHA CLUB ,DODOMA FM na wengina kwa kutaandilia show za mara kwa mara ambazo zimetusaidia kwa kipato na kuzidi kukuza mziki wa nyumbani ila pia point yangu kubwa kwa mwaka huu inarudi kwa muheshimiwa ANTONY MAVUNDE mbunge wa dodoma tunashukuru pia kwa kutamani kujaribu kuleta mapinduzi kwenye sanaa japo yanakuwa yana changamoto nyingi na hii nikutokana na watu ambao umehisi ndio wanaoweza kukusaidida kufanikisha hili ndio watu wanaongoza kuua sanaa ya dodoma nikimaanisha wanakamati kuu uliowaamini nakuwapa dhamana ndio hao hao wanaoongoza kwa kudidimiza sanaa ya dodoma wakiwa kama wadau wakubwa waliokuwa waipiganie sanaa nakujaribu kuendeleza gurudumu hili ila wao ndo waaandaji wakubwa wa matamasha mjini na mwisho wa siku wakijaribu kutugusa kujaribu kufanya kazi na sisi tukiwatajia dau wanakimbia na simu hawatopokea tena na wako tayari kuwaleta wasanii wengine na kuwalipa pesa nyingi sana na ukiwauliza huu ugonjwa utakufa lini wanakwambia wao wanaangalia biashara ....je ni lini wako tayari kufanya sanaa ya dodoma iwe biashara ...tunapoongelea mikoa ya wenzetu kila siku inaendelea kama mwanza walianza kwa kujaribu wao kama wao na kutokea watu wenye moyo kama KID BWAY nakuamisha Tanzania kuwa mwanza inaweza na mpka leo hii mwanza imekuwa ina wasanii kibao kwenye ramani ya Tanzania ...tumeshawatumikia sana wadau hawa wa dodoma na mpaka sasa wanaona sawa tu sasa sijui maendeleo yatakuja lini, muheshimiwa nilipata sana faraja kumuona mtu kama SULESH MARAH kwenye kamati mkuu maana anastahili kuitwa shujaa kwa alichokifanya kwa nguvu zake kuweza kuendesha tuzo ambazo zimeleta hamasa na changamoto kwenye mziki na ingali wanakamati hawa hawa hawakutoa sapoti pindi sulesh anaanzisha ili na baadae walishangaa juona sulesh kaendelea na tunazidi kumuombea kwa hilo je wanakamati hawa wengine wangekuwa na moyo wakweli na wakishujaa kwa ajili ya dodoma nazani hata hatua ambayo muheshimiwa ungeikuta kwenye sanaa ingekuwa iko mbali sana......nimalize kwa kusema tunakushukuru sana muheshimiwa kuwa na moyo na kuona kila sababu yakusapoti hili japo hatuzani kama linaweza kufanikiwa bila kubadilisha watu unaohisi unaweza kushirikiana nao katika hili tukimaanisha kamati kuu####