mahoajiano hayo na wakali kutoka kenye yaliwakilishwa na mmoja wa kundi hilo ambae anaitwa Bien Aime Baraza na ameweza kuzungumza vitu vingi juu ya muziki wanao ufanya pamoja na mipango yao ambao wanatarajia kuifanya.
miongoni mwa vitu ambavyo viliwekwa wazi ni pamoja na kuwa Sauti Sol kwasasa wanampango wakuachia wimbo ambao wamemshirikisha mwanadada Vanessa Mdee kutoka Tanzania na wanatamani kuutoa kabla ya mwaka huu kumalizika, pamoja na collabo hiyo pia Sauti Sol wamesema kwatanzania wamesha record wimbo na msanii wa Hip Hop Joh Makini.
Bien alipo ulizwa kwatanzania ni msanii gani ambaye anamsikiliza na kama Sauti Sol wanaheshimu kazi zao aliweza kuwataja wasanii wawili akiwemo Raymond(Rayvan) nakusema anaukubali zaidi uimbaji wake pamoja na style yake ya uandishi, Lakini pia amemtaja msanii wa singeli Man Fongo nakusema anaupenda zaidi muziki wa singeli ila anaukubali wimbo wa Ainaga ushemeji
Pamoja na hayo amesema kwasasa hawana haja ya kufanya kazi na wasanii wa nje ya Africa kwani wao wanaamini zaidi africa na wasanii wa africa ndio maana album yao ikaitwa LIVE AND DIE I AFRICA
ZAIDI BONYEZA HAPA KUSIKILIZA MAHOJIANO YOTE NA MAJIBU YA SAUTI SOL.