SLIM_SAL --WASANII WADODOMA HARAKATI ZA KWELI HAZIFANYWI KWENYE MAGROUP YA WATSAP. - NGELANGELA NEWS

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday, January 11, 2016

SLIM_SAL --WASANII WADODOMA HARAKATI ZA KWELI HAZIFANYWI KWENYE MAGROUP YA WATSAP.

msanii wa kutoka dodoma ambaye anatamba na wimbo wa Shauri yako alio mshirikisha G.nako ametoa ushauri kwa wasanii wadodoma kuhusu mambo ambayo wanaamini ni sahihi lakini kumbe yamekuwa hayana umuhimu na maslahi kwao.

akizungumza kwenye mahojiano na kipindi cha micharazo time toka 98.4 dodoma fm radio kinachoongozwa na Benedict Ngelangela Slim sal amesema wasanii wengi wa dodoma wamekuwa wakiamini kuwa kuanzisha makundi mengi ya watsap yataweza kuwasogeza kupiga hatua kuufikisha muziki mbele au msanii husika kufika mbali kitu ambacho si  kweli kwani harakati hizo si za kweli na huwa hazifiki kokote.

Slim sal ameongeza kwa kusema wasanii wengi kwenye magroup wamekuwa wakijadili vitu vizuri toka kwao na kushindwa kujadili changamoto zinazowakabili huku hata wakijadili changamoto huishia huko huko bila manufaa.

Slim amesema haitaji kuwa kwenye magroup ya watsap kwa sasa kwani hufanyika harakati zisizo na manufaa na kama mtu anataka kufika mbali ni bora kujikita kwenye muziki mzuri na kuwa na heshima kwa kila mtu na kusema hizo ndio harakati za kweli.

pia amedai kuwa kwa muda huu ukimchukua msanii anadai kuwa yeye ni mwanaharakati na ukamsimamisha ajieleze kuwa anahitaji nini kwenye muziki atakosa la kusema.

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages