Madereva wa bajaji katika
halmashauri ya Manispaa ya Dodoma wamelalamikia changamoto ya kusimamishwa ovyo
barabarani pindi wanapokuwa katika kazi zao.
Wakizungumza na kituo hiki madereva
hao wamesema wamekuwa wakifanya kazi katika mazingira magumu kwani suala hilo limekuwa likikwamisha kazi zao.
Kwa upande wake Mwenyekiti mstaafu
wa kikundi cha bajaji katika Manispaa ya Dodoma Bw.Alex Yusuphu amesema kuwa jambo hilo
limekuwa likiwapa wakati mgumu kutokana na vyombo vingine vya usafiri ikiwemo taksi kuwa
na mazoea ya kuwachukua abiria wa bajaji .
Pamoja na hayo mwenyekiti huyo
amesema wakati mwingine wasimamizi wa barabarani wamekuwa wakiwakwamisha katika
kazi hiyo pindi wanapofanya safari zao
kutoka sehemu moja kwenda nyingine
Na Nazael Mkude
Chanzo:Dodoma FM