![]() |
jacco beatz na dj mario ndani ya studio za 98.4 dodoma fm radio |
Akizungumza kupitia kipindi cha Micharazo time toka 98.4 dodoma fm radio kuanzia saa 11 hioni mpaka 2 usiku JACO amesema ameamua kuchukua uwamuzi huo mgumu wa wa kuhamisha makazi lengo likiwa ni kujikuza kisanaa na kujifunza mengi zaidi.
ameongeza na kusema watu wengi wamekua wakitafsiri vibaya maamuzi yake lakini ameweza kufanya hivyo ili kuhakikisha anaongeza ushindani kwa wasanii amabo wapo nje ya dodoma na kujua wanafanya njia gani kujitanua kimuziki pamoja na kusonga mbele kimuziki.
Alipoulizwa ni nini kimemrudisha dodoma kipindi hiki JACO amesema amekuja kufanya kazi za kimuziki za baadhi ya wasanii mkoani hapa pamoja na kusambaza wimbo wake mpya ambao unaitwa Amaizng ambao ameutengeneza yeye mwenyewe..
Kuhusu amejipangaje kumaliza mwaka JACO amesema mashabiki zake watulie vipo vitu vizuri ambavyo ataachia na itakuwa ni balaa kwenye tasnia ya muziki.
Source MICHARAZO TIME YA 98.4 DODOMA FM RADIO.