Baadhi ya wazee wa
kijiji cha kintiku wilayani bahi wametoa ushauri kwa vijana kuacha kuoa wake
zaidi ya mmoja kutoka na mabadiliko ya tabia nchi pamoja na ugumu wa maisha.
Ushauri huo wametoa wakati wakizungumza na kipindi cha
nyakati zinabadilika nakusema maisha yamebadilika stofauti na zamani kwani wazee wa zamani waliweza kuwa na wake
zaidi ya mmoja kutokana na mazingira yalikuwa mazuri katika hali ya ufugaji
pamoja na kilimo, mzee Yohana nkambi anaelezea.
Bwana Nkambi ameongeza na kusema kwasasa vijana wanakumbwa
na changamoto nyingi ikiwemo maradhi pamoja na ugumu wa maisha kama
anavyoelezea.
Nae mzee Adam Mwaluko ametoa wito kwa vijana kujishughulisha
kwa nguvu pamoja na kuwa na miradi ambayo itawasaidia kuongeza kipato pamoja na
kutunza familia.
Na benedict Ngelangela