Facebook ndio mtandao wa Kijamii ambao unatumiwa na watu wengi zaidi, Takwimu zinaonesha Duniani kuna jumla ya watu kama Bilioni 7 hivi, alafu Ripoti ya The Statistics Portal 2015 inaonesha watumiaji wa Mitandao ya Kijamii wako Bilioni 1.96, na kati yao zaidi ya 70% ni watumiaji wa mtandao wa Facebook !!
Mark Zuckerberg katupasha kuhusu mipango mingine ya Facebook, sasahivi kama ukiandika post yoyote au ukiingia kwenye ukurasa wa mtu yoyote wa Facebookunakutana na alama tatu, alama ya ‘LIKE’, ‘COMMENT’ na alama ya ‘SHARE’… lakiniCEO Zuckerberg anasema ni maombi ya muda mrefu watumiaji wa Facebook wanataka iwepo na alama ya DISLIKE, yani kama kitu hujakipenda unabonyeza tu hapo.
‘Watu wengi wameulizia kuhusu kuwepo alama hiyo, leo ni siku maalum kwa sababu natangaza rasmi kwamba tunashughulikia hicho kitu na muda sio mrefu tutakiweka kwenye majaribio‘ >>> Mark Zuckerberg.