
Juma pili hii mkoani dodoma ilifanyika show ya funga Mwezi baada ya vijana ambao wanajishughulisha na muziki wa hip hop mkoani hapa kuandaa show ambayo ili Wajumuisha pia wasanii mbalimbali.
kupitia kipindi cha micharazo time ambacho huruka kila siku kuanzia saa 11 jioni hadi 2 usiku mmoja wa wasanii ambao wanaunda kundi hilo la CENTRAL ZONE TOXIC akizungumza kwenye kipengele cha dom.com TOXIC amesema anawashukuru wadau wote kwa kuonesha kuwa wanakubali kazi ambazo wanazifanya na mpaka kuwasapoti kwa kile wanachokifanya na kukiandaa wao kama wasanii.;

Ameongezea kwa kusema ni vyema wadau wa muziki mkoani dodoma waendelee kuwasapoti vijana wao kwani dodoma kuna wasanii wengi ambao wanavipaji vya kutosha na vikubwa zaidi.

SOURCE KIPINDI CHA MICHARAZO TIME 98.4 DODOMA FM RADIO.