Taarifa zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii siku ya jana na leo kuwa msanii wa muziki wa dansi nchini,Banza Stone kuwa amefariki dunia,mwenyewe ameibuka na kukanusha taarifa hizo.
Banza amezungumza na Leo Tena ya Clouds Fm, amesema kuwa yeye ni mzima kiafya na alikuwa anaumwa kichwa lakini sasa kimetulia na kwamba taarifa hizo hazijamshtua kwa mara kwa mara amekuwa akizushiwa kuwa amefariki dunia.
‘’Sijafa nipo mzima kiafya na sina tatizo lolote huyo ananizushia kifo aende na mikoa mingine akazushe kuwa nimekufa,’alisema Banza.
Aidha mama Mzazi wa Banza amesema kuwa amekuwa akipigiwa simu nyingi na watu mbalimbali wakimuuliza kama kweli mtoto wake amefariki lakini aliwajibu kuwa ni mzima na hana tatizo lolote.