www.ngelangelanews.blogspot.com
Hata
hivyo, urembo huu huja na hatari zake ambazo wengi wanaweza
kuzichukulia poa kwa kuwa hazitokei kwa haraka ama katika muda unaoweza
kutolewa ushahidi kwa sasa.
Moja
kati ya urembo unaofanywa na wanawake wengi wa kisasa ni kuweka kope za
bandia juu ya kope halisi, kweli wengi wanakuwa na mvuto wa aina yake
wakikuangalia hasa mtoto wa kiume. Lakini hatari inayotokana na urembo
huo ni kubwa zaidi ya matokeo ya muda mfupi.
Wataalam
wanaeleza kuwa kope za bandia ambazo hugundishwa kwa kutumia gundi ya
nywele inayotumika kugundisha nywele bandia kwa wenye vipara inaweza
kuwa chanzo cha upofu wa mtumiaji.
Gundi
hiyo hupukutika taratibu sana kiasi cha kutoshtukiwa na kuelekea kwenye
mboni ya jicho ambayo ndio moyo wa ‘kuona’. Endapo mtumiaji ataendelea
kwa muda mrefu kutumia kope hizi bandia anaweza kujikuta anakuwa na
tatizo la kuona ama hata upofu wa haraka katika maisha yake ya baadae.
Hata
hivyo, hatari kubwa imeelekezwa kwa maduka ama vibanda vinatumia vifaa
vya bei nafuu ikiwemo gundi inayotumika. Ukwepaji wa gharama ama
kutokuwa na uwezo wa kutumia gharama kubwa kunamuingiza mrembo kwenye
hatari zaidi.
Kuwa mwangalifu, urembo usiwe chanzo cha kuhatarisha afya yako. Kumbuka Afya ni uhai wa mwili wako.