Baadhi ya wasanii wa Bongo fleva wakiwa kwenye mkutano.
Duh! Kama
ulikuwa unaamini kuwa lile bifu la wakali wawili wa Bongo Fleva, Nasibu
Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Ali Saleh Kiba, limekwisha, basi umenoa
baada ya jamaa hao kukutana ukumbini na kuchuniana.
Ishu hiyo ilijiri kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Double Tree Hilton jijini
Dar, juzikati ambapo wasanii mbalimbali walikutanishwa na kampuni moja
ya huduma ya simu za mkononi ili kuzungumza na wanahabari juu ya
maandalizi ya tamasha.
Waandishi wetu, wakiwa
wameingiwa na roho ya kutaka ‘ubuyu’, hatimaye muda wa kuingia Kiba
ukawadia ambapo alitinga na timu yake ya watu wanne.
Alipofika, Kiba alikaa
sehemu ya viti vya kushoto akiwa bize na mrembo mmoja wakichati kabla ya
Diamond kutimba na timu yake kubwa.
Kama ilivyo ada, macho ya
waandishi wetu yakaelekezwa kwa Diamond huku mapichapicha yakiendelea
kwa ajili ya kutupia kwenye mitandao ya kijamii.
Kila msanii aliyefika
kwenye ukumbi huo alianza kutoa salamu kwa mtu anayeona anafaa kwake,
lakini cha kushangaza mastaa wawili Kiba na Diamond walishindwa kupeana
hata mikono huku kila mmoja akiwa ameuchuna na kampani yake.
Hata hivyo, wakati ulipofika wa wasanii kujitambulisha mbele ya wadau,
mastaa hao walitahadharishwa kwamba atakayeanza au atakayekuwa wa mwisho
kujitambulisha haina maana kwamba yeye ndiye mkubwa zaidi kistaa.
Katika kujitambusha, Kiba ndiye aliyeanza huku kila mtu akitamba kufanya vizuri kwenye kila shoo zitakazofanyika mwaka huu.
Hakuna aliyekuwa tayari kumzungumzia mwenzake