kamanda wa polisi wa mkoa wa Mbeya Diwani Athuman ............................................................. Taarifa kutoka Tunduma mkoani Mbeya zinadai kuwa hali si shwari katika eneo hilo kutokana na kuzuka kwa vurugu kubwa zinazodaiwa kusababisha na masuala ya kiimani ya nani achinje kati ya mkristo na Muislam . Mwandishi wa mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com kutoka Tunduma mkoani Mbeya Moses Ng'wat anaripoti kuwa vurugu hizo zimeanza majira ya saa nne asubuhi kwa makundi ya vijana kuandamana mitaani na kuvutana kuhusu uamuzi wa viongozi wa dini ya kikristo Tunduma kuandika barua kwa mkuu wa wilaya kutaka kuruhusiwa kuchinja wakati wa pasaka. Alisema kuwa kabla ya ijumaa kuu viongozi hao wa dini ya Kikristo walikutana na mkuu wa wilaya ya Momba Abuud Saibea ambae aliwataka kuwasilisha barua rasmi ya kufanya hivyo . Hata hivyo inaelezwa kuwa vurugu hizo za leo hazina mahusiamo ya moja kwa moja na masuala ya dini kwani wanaoshiriki katika vurugu hizo ni vijana wapiga debe ambao baadhi yao wamechanganyika na vibaka kwa lengo la kuchafua hali ya hewa . Kwani suala la uchinjaji ambalo lilifanyika siku ya Pasaka halikuwa na mvutano wowote baada ya wakristo kuchinja katika bucha zao na waislamu hao kuchinja katika mabucha yao na kila mmoja kufanya biashara kwa kupata wateja wake kama kawaida . Ila katika hali ya kushangaza ni baada ya leo kuibuka kundi hilo la vijana wanaofanya kazi katika stendi na vijiwe mbali mbali kuanzisha vurugu kiasi cha polisi kuingilia kati kwa kutumia mabomu ya machozi na kuwatawanya wananchi waliokuwa wamekusanyika maeneo mbali mbali . Kutokana na vurugu hizo mpaka wa Tunduma ambao unaingia nchi za kusini wa Tanzania ulifungwa pamoja na magari yaliyokuwa yakitoka Sombawanga pia kuzuiwa kuendelea na safari hadi hali hiyo ilipotulia mida hii saa 8 mchana baada ya kamanda wa polisi wa mkoa wa Mbeya Diwani Athuman kufika eneo hilo. Taarifa zisizo rasmi ambazo bado kuthibitishwa na jeshi la polisi zinadai kuwa mtu mmoja ndie amejeruhiwa japo hakuna madhara makubwa yaliyojitokeza . na francis godwin |
Post Top Ad
Responsive Ads Here
Wednesday, April 3, 2013

Home
Unlabelled
MPAKA WA TUNDUMA MBEYA KWA MUDA WAFUNGWA KWA MUDA POLISI WATUMIA MABOMU
MPAKA WA TUNDUMA MBEYA KWA MUDA WAFUNGWA KWA MUDA POLISI WATUMIA MABOMU
Post Bottom Ad
Responsive Ads Here
Author Details
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.