Dar es Salaam. Kocha wa Yanga, Ernest Brandts amewaonya wachezaji wote wa kikosi hicho wanaopuuzia mazoezi wakijiona tayari wameshapata ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Yanga kwa sasa ndiyo inayoongoza msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 48 ikifuatiwa na Azam yenye ponti 37, ambapo timu zote hizo zimebakiza mechi sita kumaliza ligi hiyo. Brandts alisema kuwa, hatawavumilia wachezaji wa aina hiyo katika kikosi chake na endapo atawabaini atawachukulia hatua kali za kinidhamu. Bado hatujachukua ubingwa hivyo sioni sababu ya wachezaji kuanza kutegea mazoezi, wanachotakiwa ni kuhakikisha wanajituma vilivyo katika kipindi hiki ili tutimiza lengo letu kwa asilimia mia moja, alisema Brandts. Alisema, Tunahitaji kushinda mechi zetu zote zilizobakia hivyo kwa sasa uvivu hautakiwi, nitawachukulia hatua kali wale wote watakaobainika kutokujituma mazoezini kwa kuona kuwa tayari tumeshapata ubingwa, alisema Brandts. Alisema kwa sasa kikosi chake kinaendelea kujifua tayari kwa kukabiliana na Polisi Morogoro, Jumamosi ijayo katika mchezo wa Ligi Kuu utakaofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro. |
Post Top Ad
Responsive Ads Here
Monday, March 25, 2013

Home
Unlabelled
KOCHA WA YANGA AWAPIGA MKWARA WACHEZAJI
KOCHA WA YANGA AWAPIGA MKWARA WACHEZAJI
Post Bottom Ad
Responsive Ads Here
Author Details
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.