Mzee Kingunge (87) alikuwa akitibiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akiuguza majeraha ya kushambuliwa na kung’atwa na mbwa akiwa nyumbani kwake.
Katika enzi za uhai wake Mzee Kingunge alikuwa mmoja wa viongozi wa muda mrefu wenye ushawishi na waasisi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) hadi alipojiuzulu kutoka kwenye chama hicho Oktoba 2015.