Msanii jaco beatz ameachia wimbo wake hivi karibuni wakuitwa baby
ambao kamshirikisha msanii mwenzake anaetokea Dodoma wakuitwa Moni cntralzone
anaetamba na wimbo wake wa Mwaaa ft Country Boy, kitu cha kupongezwa kwa hawa
vijana ni kuachia wimbo wenye mahudhui mazuri na video kali kiujumla wimbo
umejaa vizuri sana.
Sasa hapo kwa wakazi wa Dodoma ishu sio Jaco Beatz kuachia
wimbo na Moni maana wote wawili wanafahamika na katia mkoa huu unaweza
kuwasimamisha nakuwaweka kwenye meza moja ndio maana watu hawajashtushwa sana
Moni kuwekwa kwenye wimbo wa jaco zaidi wamepongezwa kwa kiasi kikubwa kuwa
wameungana kupeperusha bendera ya mkoa wao vizuri.
Lakini kwa nje ya mkoa wadodoma huwezi pinga kuwa Moni ni
mkubwa sana kuliko Jaco beatz tena kamuacha mbali hawezi kumgusa hata kwenye
unyayo kwani Moni anangoma nyingi zimehit hadi nje ya Tanzani nakolabo za
wasanii wakubwa kitu ambacho kinamtambulisha Moni kuwa ni msanii wa kitaifa sio
msanii wa Kanda Fulani.
Jaco Beatz kufanya kazi na Moni ni jambo la kheri kwakwe
kwani kwasasa anaweza kuwanyakuwa mashabiki wa moni wakawa upande wake kwani
kuna watu wataupakuwa wimbo kwasababu wameliona jina la Moni Centozone
wakaangalia Moni alichofanya ndipo wanapata nafasi ya kumsikia jaco alichoimba
kwaio ni credit kwa Jaco beatz.
Pili Moni kwasasa anaconnection ya watu wengi kwaio ni rahisi
Moni kumsaidia Jaco kuwafikia wadau wengi wa muziki kwasasa hususani watu
waradio na Tv, pamoja na wadau ambao wanaweza kuwapiga tafu kwenye kusambaza
ngoma zao,kwaio ni vyema kwasasa Jaco akajinyenyekeza kwa Moni kwani akileta
jeuri anaweza akajikuta akirudi nyuma nakukosa msaada ni vyema akutulia
nakumuheshimu Moni kama mkubwa kwake kwenye muziki ili nae afikie lengo kwani
hata Moni alishawahi kujinyenyekeza kwa watu ndio maana akafikia hapo alipo.
SASA Jaco Beatz mgongo uliobebwa hata kama haukutoshi
jishikize hapo hapo sasa ukiruka ruka nakuchana mbeleko hiyo utarudi nyuma na
mafanikio utayasikia kwenye Bomba.
TAZAMA VIDEO YAO HAPO.
@ngelangelanews.blogspot.com