BIORN ENTERTAINMENT KUHUSU KUTOA WIMBO ILI KUZIMA WIMBO WA JACO BEAT FT MONI, WAMEJIBU HAPA.. - NGELANGELA NEWS

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wednesday, January 24, 2018

BIORN ENTERTAINMENT KUHUSU KUTOA WIMBO ILI KUZIMA WIMBO WA JACO BEAT FT MONI, WAMEJIBU HAPA..

Mwaka 2018 umeanza kwa kasi sana kwenye kiwanda cha muziki ndani ya mkoa wa Dodoma kwa nyimbo zenye ubora wa hali ya juu kuachiwa toka kwa wasanii husika wanaofanya muziki wa Bongo fleva kwani nyimbo zao zimepokelewa kwa kiasi kikubwa kwa mashabiki wa muziki.
Image result for JACO BEATZ
Hivi karibuni msanii na producer wa muziki kutoka mkaoni Dodoma JACO BEAT ameachia wimbo ambao wamemshirikisha msanii mwenzake toka Majengo sokoni Moni Centralzone wimbo huo ambao umepiwa jina la baby ambao ni moja ya nyimbo kubwa kwasasa.

Jaco beatz ambaye ni mmiliki wa label ya Peremende Music ndie msanii pekee ambaye amekuwa akionesha ushindani mkubwa kwenye label ya biorn entertiment nayo inapatikana mkoani Dodoma, na baada ya kuachia wimbo wake huo wa baby yalianza kuzuka maneno huwendawapinzani wake wataachia wimbo ili kuzima upepo alioupata Jaco Beat na wimbo wake wa Baby.

Kilichotabiliwa ndicho kilichotokea kwani Biorn waliachia wimbo kutoka kwa wasanii wao wanao wamiliki ambao ni Davy Cobra na Papaa nakuachia wimbo unaitwa Kama mbele ambao umeambatana na video moja kwa moja kitu ambacho kilifanywa na msanii Jaco Beat katika mfumo wake wakuachia wimbo wake.

wakati wakiachia wimbo wao huo kupitia kipindi cha Micharazo time toka 98.4 Dodoma fm radio uongozi wa Biorn walipoulizwa swali kuhusu tuhuma hizo wamejibu nakuelekeza kwakusema wakati wanapanga kuachia ngoma yao hawakuwaza kuwa kuna msanii mwingine ataachia wimbo lakini imetoka kunamsanii amewahi kutoa wimbo wake kwaio hawawezi kuacha kuendelea na kazi zao kwaajili ya kazi ya mtu mwingine.

Aidha Dir wa Biorn  dir Aminy amesema kama wao wanaambiwa wametoa wimbo ili kuzima kazi zao sio kweli lakini inabidi watu watambue kuwa ushindani kwenye muziki na hauwezi kupingwa hata siku moja ila kwaupande wao wameachia wimbo kutokana na kuona ni muda sahihi wakumuachia msanii wao ila kama jaco beat ataona ni kweli nae auzime wimbo wao.

Sanjari na hayo Frank Music amempongeza Jaco Beat kwakuachia wimbo mkali wenye video kali na upande wao waliusapoti wimbo huo kwakuupost kwenye mitandao yao yakijamii.

EBU ZITAZAME NYIMBO ZOTE MBILI MBILI HAPA.
HII YA JACO FT MONI CENTROZONE.

NAHII NI YA DAVY COBRA KUTOKA BIORN.



Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages