MUDA HAUKUSUBIRI DADA ANGU, UTADANGA HADI LINI? STORY BY EVAR MOSES. - NGELANGELA NEWS

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wednesday, July 19, 2017

MUDA HAUKUSUBIRI DADA ANGU, UTADANGA HADI LINI? STORY BY EVAR MOSES.

Wewe ni msichana mzuri, unapenda kwenda na
wakati. Umeshaanza kutumia vilevi. Tena vile
laini ambavyo ukinywa leo unaweza kulewa
kesho. Una mahusiano na John. Lakini unampenda sana Simon. Japo mvulana aliyekutoa bikira ni Raby
lakini toka muachane humuhitaji tena kwakua
unamuona mshamba na unaona kabisa kua
ulikosea njia kuwa nae. Sponsor Molito ni baba unaye muheshimu sana.Kwakua uki date nae tu basi unarudi na mkwanja mrefu nyumbani.
unaanza kufanya photoshoot za nusu uchi na
Image result for girls crying

John hana pesa nyingi, ila bishoo. Ana Dred na
kifua kipana. Anashinda gym kwa sababu yako ili
u enjoy ukiwa nae. Simon ndio mvulana anaye julikana na rafiki zako wengi kwakua ndio mvulana ambaye unashinda nae muda mrefu. Hivyo umemuaminisha kua unampenda yeye peke yake.

Simon ndio mvulana ambaye unaweza hata
kumpost kwenye mitandao lakini Caption zako za
kawaida sana zisizoonyesha dalili zozote za
mahusiano. Upo na marafiki zako wapatao wanne ambao wote life style yenu ndio hiyo. Kila mkilala mchana mnawaza usiku muende club gani au wapi kuna pub nzuri ili mlewe.


Unaishi na mama yako na wadogo zako
wanasoma. Mama hana usemi kwako kwakua
ukitoka kwa Sponsor Molito unamtupia laki 2.
Mama anakuruhusu ukapumzike. Na simu yako
ikiita anakuletea ndani na kukuamsha kwa adabu.
Kiufupi mama yako hana kauli juu yako kwakua
wewe ndio tegemezi. Shopping yako ni laki 3 kwenda mbele. Hurudii nguo mara tatu. Usisikie simu mpya imetoka. Tayari unayo. Kwenu hamna gari lakini
umeshajifunza na unatembelea magari Zaidi ya
matatu lakini huna kadi hata moja. Umepanga nyumba nzima na huna kazi mjini. Ofisi yako ni simu na sauti nzuri ya kutokea puani.


Miaka haisubiri. Ulikua na miaka 20 na miaka
saba baadae unakua na miaka 27. Hushtuki. Poda zinaanza kudunda na vipodozi vinaanza kukataa kushika kwenye ngozi yako. Unaamua kubadilisha cream na kutumia zile kali kali ili ngozi ikubali.

Unakua mweupe sana. Macho nayo yanapoteza
nuru. Huwezi tembea kwenye jua kali. Muda wote
kope za bandia ndio mlinzi wa muonekano wako.
Sponsor Molito nae anahitaji kuwa na watoto
wabichi wa miaka 20. Wewe age imeshakutupa
mkono. Anakuona wa kawaida. Huna maajabu
tena. Anakuacha na kukupa wakati mgumu wa kutafuta Sponsor mwengine.


Inakua ngumu kuwapata kwa natural face,unaanza kufanya photoshoot za nusu uchi na
editing nyingi ili wachuuzi wanase. Wananasa watoto wa facebook na Instagram wafuga dread na wanyoa viduku. Hao huwataki. Stress zinapanda unaanza kumlazimisha Simon akave nafasi ya Molito. Simon hana uwezo. Unampiga chini unabaki na Serengeti boy wako John. Huyo anapendwa na wasichana wengi, unamfumania na kuachana nae kwa matusi.
Unabaki Single, huna danga wala bwana. Rafiki
zako ukiwapigia simu ni vizinga tu na kuwaomba
wakutoe out.. huna Ishu. Unalala tu usiku wakati
ulikua unajiita POPO.


Rafiki zako wanakupitia na magari yao ambayo
hawana kadi nayo wanakutoa. mkitoka ni wao tu
ndio wanatumia pesa zao. Baada ya muda
wanakuchoka, Wanaanza kukutenga na kukuzimia
simu. Huwezi panda daladala kwakua mtaani unaitwa Cash Madame. Unaanza kupanda pikipiki kila mahali uendapo. Huna pesa za kulipia usafiri kila siku. Unaamua kutembea na dereva boda boda ili upate usafiri wa bure. Huyo hakutoshi kwakua wewe una gaharama sana. Unaamua kumpa penzi mangi wa dukani ili vitu vidogodogo uwe unachukua bure, Mangi hana siri, anakutangazia kuwa unamtaka na kuwa skendo kwako. Unaamua kujifungia ndani skendo ipite. Laahaulaaaaaaaaa!
Unakuja Kutahamaki. Unafungua friji kuna maji tu,
dawa ya meno imeisha, Gesi imaisha, luku nayo
inakaribia kuisha, dukani kwa shirima mnadaiwa
laki 2. Kodi ya nyumba inakaribia. Unamuita baba
mwenye nyumba unampa penzi. Anakuongeza
miezi mitatu.. Kuja kutahamaki wewe unaishi kwa kufanya mapenzi na kila aina ya mtu kwakua tu umeamua ku fake maisha yako.


Yanini yote dada zangu?
Jikubali kua wewe unaweza kutoka kimaisha na
kuisaidia familia yako kwa njia salama kabisa bila
kuutumia mwili wako. Hayo madanga huwa hayazeeki bali wewe unayedanga ndio unapitwa na wakati. Hayo madanga wanapenda wasichina wenye
miaka ishirini. Wewe ukipita basi atatafuntwa mwengine. Utaishia kutunza makabati ya kichina wenzako wakiolewa na wewe ukabaki na uzuri wako wa dukani.


Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages