Nimekutana na picha kadhaa ujenzi wa ofisi za Dodoma kwanza kwaajili ya wasanii wa Dodoma.
Ofisi hizo kujengwa ilikuwa ni ahadi ya mbunge wa Dodoma mjini Mh Anthony Mavunde kwa lengo la kuwasaidia wasanii wa muziki, filamu pamoja na Sanaa mbalimbali.
Erick ni kiongozi kwenye kamati iliyotolewa na Mavunde kwa lengo kuwafanya wasanii mbalimbali wanakutana na kamati hiyo kufikisha malalamiko yao.
Erick ametumia mtandao wa whatsap kupost picha za ujenzi wa ofisi hizo zikiendelea na ujenzi nakusema ujenzi wa ofisi hizo upo katika mitaa ya Mapinduzi Bahi road.