miongoni mwa vitu ambavyo vilikuwa nikilio kwa wasanii wadodoma ni kwanini nyimbo zao hazisikiki kwenye club na Pub za mkoani dodoma? na ukweli unaweza kwenda club kuanzia juma tano hadi jumapili usisikie kabisa ngoma za wasanii wa dodoma zikipigwa huku swali likiwa halijulikana kama ni wasanii wenyewe hawajui umuhimu wakupeleka ngoma zako kwenye club mbalimbali ama laah au madj na uongozi wa club hawazitafuti na hawazijui kabisa.
 |
dvj hunter |
sasa kupitia kipindi cha micharazo time toka 98.4 dodoma fm radio kinachoongozwa na Benedict Ngelangela alisikika mmoja wa viongozi na Dj kutoka Maisha Club Dodoma DVJ HUNTER akitangaza kuwa kuwa kila juma pili ya kutakuwa na list ya ngoma kali tatu toka Dodoma zawasanii wadodoma na lengo kubwa likiwa kuitambulisha sanaa ya dodoma kwa wadau tofauti na wapenda burudani.