![]() |
1 |
miongoni mwa wasanii ambao walikua hawana majina makubwa mkoani dodoma ni SIMAO ila baada ya kujiunga na BIORN jamaa alifumuka kama upepo nakutishia hali ya hewa kwawasanii wengine baada yakuachia ngoma yake ya made it aliofanya na msanii mwenzake MONI na iliambatana na video kubwa.
baada ya muda mfupi tulisikia mambo yakibadilika na story zilizagaa kuwa msanii SIMAO hayupo tena kwenye labe hiyo ya BIORN ENTERTIMENT kitu ambacho wahusika hawakuweza kutoa kabisa taarifa yoyote juu ya tetesi hizo.
![]() |
simao |
sasa kupitia kipindi cha Micharazo Time toka 98.4 dodoma fm radio kikiongozwa na Benedict Ngelangela viongozi wa label hiyo walitupatia Exclusive majibu juu ya suala hilo ambalo lilizua mjadala mkubwa katika mahojiano hayo.
Franck Musiq na Moh ni viongozi wa label hiyo na wamesema kuwa SIMAO nado ni msanii wa BIORN kwasababu anamkataba wakikazi ambao haujamalizika mpaka sasa, walipoulizwa kwanini haonekani wakiwa pamoja Franck musiq alijibu nakusema kila kitu kina muda wake kwaio lazima kazi zingine ziendelee kwani huwezi kuwa na msanii mmoja muda wote na wao kama BIORN hufanya kazi kwa ratiba kwaio ratiba moja ikimalizika zingine zinaendelee pia wanfoleni yawasanii kibao ambao wanahitaji kufanya nao kazi na kazi zao zinatarajiwa kutoka muda si mrefu.
pia kuhusu kama ni kweli walimtema SIMAO label hiyo imekana kufanya jambo hilo na wakakiri kuwa wapo sawa na msanii huyo ila anaruhusiwa kufanya kazi na studio zingine ambazo zipo juu na zenye uwezo wa hali ya juu au lavel sawa na BIORN ENTERTIMENT.