Jeshi LA polisi mkoani Arusha linawashikilia watu wawili Frank Mkumbi Sanga miaka 25 kabila Mnyiramba na ni mkazi wa Tanga pamoja na Kanuti Benedict miaka 32 mwendesha piki piki kabila mchaga na ni mkazi wa Shamsi wilaya na mkoa Arusha.
Wawili hao wamekamatwa wakati wakisafirisha madawa hayo kupitia piki piki ya miguu mitatu aina ya Toyo yenye No za usajili Mc 203 AHJ ambayo bangi izo zilikuwa zikisafirishwa kuelekea mkoani Tanga na ilikuwa imefichwa ndani ya magunia ya karoti.
Jeshi LA polisi mkoani hapo linasema asante kwa wote waliofanikisha kukamatwa kwa watu hao.
Imetolewa na kamanda wa polisi mkoani Arusha Naibu Kamishna wa polisi DCP Charls Mkumbo.
Na Veronica Emmanuel Grevas
TAZAMA PICHA.