MSANII WA FILAMU SONNATHA NDUKA MKALI WA KESHO YANGU AMKINGIA KIFUA SULEISH MARAH. - NGELANGELA NEWS

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wednesday, November 2, 2016

MSANII WA FILAMU SONNATHA NDUKA MKALI WA KESHO YANGU AMKINGIA KIFUA SULEISH MARAH.

Msanii wa filamu kutoka  mkoani Dodoma Sonatha Nduka ambaye kwasasa anatamba na filamu yake iitwayo KESHO YANGU amesema game la filamu kwasasa kutoka mkoani dodoma ni kubwa endapo mtu akiwa serious na kazi hiyo na akihitaji kuweka nguvu anaweza akafanikiwa.

Sonnatha ameyazungumza hayo kupitia kipindi cha micharazo Time Toka 98.4 Dodoma fm radio wakati akijibu swali la mtangazaji wa kipindi hicho Benedict Ngelangela kuwa hali ya soko la Dodoma likoje.
sonnatha nduka

kwaupande mwingine Sonnatha alipoulizwa kwanini wasanii waliopitia kwa Director mwenye jina kubwa nchini anaetokea Dodoma Suleish Marah humsema vibaya kuwa amekuwa akiwapa nafasi baadhi ya wasanii amabo yupo karibu nao zaidi, Sonnatha amejibu si kweli bali Suleish ni mtua anae ijua kazi yake na humpatia mtu kazi yakufanya kutokana na maudhui ya story na sehemu anayo fit na hana upendeleo.

Pamoja na hayo ameongeza na kusema wasanii wengi wamekuwa na hamu yakutoka kwa haraka bila kuweka vipaji vyao vizuri ndio maana hujitoa nakutoa maneno ambayo si sahihi kwa baadhi ya watu, akijitolea mfano yeye Sonata amesema amekaa kwa Suleish takribani miaka mitatu lakini hajawahi kucheza moview watu wamekuwa wakija wanapata nafasi lakini hajawahi kulalamika kwani aliamini siku yake itafika na mpaka sasa ndio ametoa movie yake iliyo chini ya Suleish na inafanya vizuri kwasasa.

Sonnatha nduka amewataka wasanii wa movie Dodoma kuwa wavumilivu watayafikia mafanikio.


Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages