Ukizunguka kwenye makundi mengi ya watsap vijana wa mkoa wa dodoma hususani wanao jihusisha na masuala ya burudani strory kubwa ni WHO IS MALKIA WA DOM? wakijaribu kuweka mada ambazo zikiididscuss account ya instagram ambayo inatumia jina la MALKIA WA DOM.
account hii imekuwa gumzo kutokana na mada pamoja na picha ambazo huzipost mmiliki wa account hii ambaye hajulikani mpaka sasa lakini kinacho endelea ni kila mtu kutaja mtu anae muhisi kuwa ndiye mmiliki wa account hiyo.
Account hii imefanikiwa kuwa maarufu kwa muda mfupi kutoka na mambo ambayo hupostiwa humo kugeuka kuwa gumzo mitandaoni huku baadhi ya watu wengine huishia kutukanana kwa kuyavulia maji yasiyo wahusu.
SASA BASI unaambiwa usiombe upostiwe au uonekane sura yako kwenye account hii ni balaa moja unaweza ukasifiwa au ukaliona joto lajiwe, ila kwa kukandiwa ndio mara nyingi zaidi kwani mmiliki wa account hiyo fomula yake inaonekana kuwa ni lolote lililo kaa ovyo kwenye tasnia mbalimbali mkoani dodoma. huku zaidi akidili na wanamuziki pamoja na waigiza na wengine wanao shabiana kwenye hayo mambo.
Wapo wengi waliloliona joto la jiwe akiwemo ONESIX msanii wa muziki akituhumiwa kupiga show mbaya kwenye tamasha la Dodoma Festival 2015 lililo andaliwa na kituo cha radio Dodoma Fm radio, Mambo si mambo ndipo msanii wakuitwa RHODA nae alikumbana na jinamizi hilo kwa kuambiwa hajui kuimba na kusababisha mpaka kijana huyo kutangaza kuacha kuimba tena baada ya hayo kutokea ndipo mtangazaji wa radio toka Rasi fm alipo ingilia kati na kuanza kutoa matusi kwa mtu ambaye hata hamjui kwenye mitandao ya kijamii eti anamfahamu uyo mmliki wa account hiyo lakini mpaka sasa hakuna jibu lolote alilolitoa ni sawa alikuwa anatwanga maji kwenye kinu.
jinamizi hilo pia lilitua kwa muigizaji wa wa bongo movie kwakushutumiwa kuwa alirepost picha ya show y dodoma festival wakati muda umepita huku waandaji wa show hiyo wakila dongo kwa kumita rachel ni super star wakati hata jamatini hajulikani duuuh ni balaa.
hayo ni baadhi kati ya mambo mengi ambayo huandikwa kwenye account hiyo.
Account hiyo imesababisha baadhi ya watu kutoelewana kama Sonnatha Nduka toka nyemo fm VS Onesix, huku Raph tz VS Dizzy swags.
wapo baadhi ya watu wametokea kuipongeza account hiyo kwa kuandika ukweli juu ya madudu yanayoendelea kwenye jamii na tasnia mbalimbli dodoma huku wengine wakidai inadhalilisha watu kwani hutumia majina ya watu bila taarifa pia hutumia picha za watu bila kuwajulisha kitu ambacho ni kosa kubwa kisheria.
Ukweli ni kwamba hakuna anae penda kukosolewa kwa mabaya bali watu wanapenda kusifiwa muda wote sasa basi anae penda kukosolewa hawezi kuichukia account hiyo y a Malkia WAdom kwani ipo kwa lengo la kuwarekebisha watu wafanye vitu vizuri.
LAKINI nawe mmiliki wa aacount hiyo uwe unajitahidi kutumia lugha nzuri kidogo ili wenzako wasikuchike maana duuuh ni tatizo kidogo ambalo husababisha mpka matusi kumwagika pia kitendo cha kutumia picha za watu bila taarifa hilo nalo ni tatizo. ILA SI MBAY NA JUA UNALENGO ZURI LA KUKUZA TASNIA YA DODOMA DATS Y UNATOA MADUDU UYAONAYO. ILA KITAA WANATAMANI WAKUJUE WE NI NANI maana kuna watu wanabebeshwa mizigo si yao mkuu, pole kwa SONNATA ABDALA, DIZZY SWAGS na wengine ambao wameambiwa ni wahusika wa aacount hiyo.