ALICHO ANDIKA JANUARY MAKAMBA JUU YA KIFO CHA DEO FILIKUNJOMBE WAWEZA TOKA MACHOZI - NGELANGELA NEWS

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday, October 16, 2015

ALICHO ANDIKA JANUARY MAKAMBA JUU YA KIFO CHA DEO FILIKUNJOMBE WAWEZA TOKA MACHOZI

baada ya kutangazwa kutokea msiba wa Filikunjombe baadhi ya watu kupitia mitandao ya kijamii wamekuwa na mengi ya kuzungumza.
january makamba

lakini maneo haya ya aliandika January Makamba yamewagusa wengi zaidi na kuweza kufikisha comment nyingi zaidi kupitia ukurasa wake wa facebook.

SOMA ALICHO ANDIKA KWENYE UKURASA WAKE WA FACEBOOK.
Deo filikunjombe enzi za uhai wake
Siku mbili kabla ya jana, Deo Filikunjombe alinipigia simu akitaka tuzungumze kuhusu mikakati ya ushindi wa CCM. Tukaongea kwa saa nzima. Akawa anawahi kwenye shughuli nyingine. Leo naambiwa hatunaye. Siamini. Siamini kwasababu bado nasikia sauti yake kichwani mwangu.
Nilimjua Deo mwaka 2010, wakati anaanza kugombea Ubunge. Nilikuwa sijawahi kukutana naye kabla ila alinitafuta kuomba tushauriane kwasababu baadhi ya makada walikuwa wanataka kumwekea mizengwe asipitishwe (hata baada ya kushinda kura ya maoni) kwasababu walikuwa wanadai eti ni “mhuni”. Tukashauriana. Mizengwe ikashindwa. Tukawa marafiki.
Kuna siku, mapema mwaka huu, alinipigia bila kutegemea akisema kwamba anataka kunipa a portable PA system ili niwe naitumia jimboni. Sikuwa nimemuomba wala sikuitegemea. Alifanya kwa mapenzi.
Jana usiku, wakati natoka Handeni kumzika Dkt. Kigoda, habari za ajali ya helikopta ya kampeni ya CCM zilienea kwa kasi, huku wengine wakisema kwamba Kinana yumo, Mwigulu yumo, na hata mimi nimo kwenye hiyo helikopta. Nikafuatilia viongozi wote waliokuwemo kwenye helikopta zote tulizokodisha rasmi kama Chama. Kila mmoja akasema yuko salama. Tukaripoti kuwatuliza wanachama. Tukaomba Mungu tetesi za ajali ya helikopta yoyote ile zisiwe za kweli. Hatukukubaliwa. Tetesi zikathibitishwa kwamba Deo alikuwa na helikopta aliyokodi binafsi tofauti na zilizokodishwa na Chama, na kwamba ni kweli ilipata ajali na wote waliokuwemo wamefariki.
Mwezi wa tisa, tulikaa na Deo kwa masaa mawili ofisini kwa Katibu Mkuu wa Chama, Ofisi Ndogo Lumumba. Alikuwa na ushauri mzuri kuhusu kampeni na ushauri wake ulifanyiwa kazi. Alipenda watu wake. Alikuwa na msimamo. Ameondoka mapema. Tunaambiwa tusihoji matakwa ya Mungu lakini kuna nyakati inakuwa ngumu. Pole pia kwa Ndugu Jerry Silaa kwa kuondokewa na baba mzazi.

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages