Akizungumza na mwandishi wa habari wa mtandao huu kupitia 98.4 dodoma fm radio kipindi cha Micharazo time KOKU ametoa mapya na kusema alikuwa anafanya muziki kwa muda mrefu kwa kujificha bila wazazi wake kujua kwani walikuwa hawahitaji KOKU Kufanya muziki wa kidunia kutokana na waokuwa na Imani ya kidini zaidi huku wakihitaji msanii huyo kuwa mwimbaji wa nyimbo za Dini.
KOKU kwa akizungumza kwa tabasamu na furaha isiyo kifani amesema wazazi wake kwasasa wamemruhusu kufanya muziki huo ila wamemkanya kuto kuiga mambo mabaya ambayo yatawakwaza wazazi pamoja na jamii inayo mzunguka.

NUKUU
""""nipo tayari sasa kufanya muziki maana wazazi sasa wameniruhusu kuimba, nilikuwa nashindwa kabisa kwenda kwenye show za usiku lakini sasa namshukuru Mungu wazazi wamekubali.""""
SOURCE... 98.4 dodoma fm radio kipindi MICHARAZO TIME