Mkurugenzi wa Benchmark Production ambao ni waratibu wa shindano la kusaka vipaji la Bongo Star search Ritha Paulsen “Madame Ritha”amewaka na kusema msanii wa bongo flava Ney wa Mitego anatafuta kick ili aendeshe maisha yake.
Madame Ritha akizungumza kwa hasira baada ya kumtupia swali la kutakiwa kujieleza kuhusiana na tuhuma za kumdhulumu mkwanja mshindi wa mwaka uliopita Walter Chilambo kama ilivyoimbwa na Ney kwenye wimbo wake wa salamu zao amesema hiyo ni style ya msanii huyo kutafuta namna ya kuishi kwa kupata kick kupitia migongo ya watu.
Anasema msanii huyo hana namna ya kutengeneza nyimbo zake zikapendwa zaidi ya kutumia style hiyo ya kuwasema watu hata kwa vitu ambavyo havina ukweli wowote ili maisha yake yaweze kwenda.
“We unaona inawezekana sisi kufanya hicho kitu,si tungekuwa tumeshafungiwa na Basata(Baraza la sanaa la Taifa) kuendelea na shindano hilo,mbona bado tupo tunaendelea?Huyo Ney anazungumza vitu ambavyo havipo kabisa muulize Walter mwenyewe atakwambia kama kapewa au hajapewa”Alisema Madame Ritha.
![]() |
Ney na Madame Ritha |
Washiriki wa BSS mwaka huu walioingia fainali |
Hivi karibuni Ney wa Mitego alitoa sigle yake ya Salama zao ambayo ndani yake amemtaja Chilambo mshindi wa BSS mwaka uliopita kuwa pamoja na kushinda hajapewa zawadi yake ya shilingi milioni 50 na ndio maana amechoka na mpaka sasa hana hata baiskeli,jambo lililozua gumzo
SOURCE MAMUAFRIKA