Msanii wa Muziki Abdul Aziz kwa jina la sanaa anafahamika
kama WYSE1 ambaye anafanya kazi chini ya usimamizi wa msanii mwenzake Ben Pol
amefunguka juu ya ujio wa nyimbo zake mpya pamoja na kurudia nyimbo za wasanii
wengine.

Akizungumza na kipindi cha Micharazo Time kutoka 98.4 Dodoma
Fm Radio @wyse_tz amekanusha tetesi za kuwa @iambenpol amekuwa akijependelea
katika suala la kuachia nyimbo kwani amekuwa akitoa nyimbo nyingi kuliko msanii
wake, @wyse_tz amesema si kweli kama anabaniwa kwani vyote hivo vilisababishwa
na yeye kuwa masomoni lakini kwasasa amesjipanga kuwafurahisha mashabiki.
Upande wa kuhusishwa kumtelekeza mpenzi alikuwa nae Dodoma
WYSE amesema kwasasa anampenzi mpya ambaye ni mtu maarufu nchini na wamepanga kutoyaweka
wazi mahusiano yao, kama mwanamke huyo ni msanii wa muziki, video queen au
muigizaji wa filamu wyse1 hakuwa tayri kuelezea nakusema watu wake wa nyuma
waliachana ka watu wengine wanavyoachama.
@wyse_tz Ameyataja mafanikio aliyoyapata baada yakurudia
wimbo wa msanii @symplysimi wimbo wa joromi ni pamoja na kutafutwa na msanii
huyo ambaye alimtaarifu kupenda sauti yake na tayari wameshaanza kuandaa wimbo
ambao Wyse1 ataimba na msanii anaesimamiwa na SIMI.
SOUCE: MICHARAZO TIME 98.4 DODOMA FM RADIO
@benedict_ngelangela.