
akizungumza na Dodoma fm radio kupitia kipindi cha micharazo time Lava lava amesema anashukuru Mungu kwakuweza kumsaidia kutoa ngoma zake na kupokelewa vizuri kwa mashabiki zake hususani wanawake.
Aidha lava lava amesema kiukweli kwa upande wake alipokea vizuri kauli ya Ally kiba kuwa anapenda sana kusikiliza wimbo wake wa Bora tuachane kwasababu kipindi anakuwa alitamani sana kufikia ukubwa wa Ally kiba.
Kuhusu kitu asichokipenda kwenye muziki wa bongofleva Lavalava amesema kitu asichokipenda ni uwepo wa timu za muziki kwani mara nyingi zimekuwa zikileta mpasuko wakimuziki na watu kuchukiana hata kama wakifnaya kazi nzuri.
kwasasa Lavalava ameachia nyimbo anatamba na wimbo wake KILIO.